Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza kutoka Gorgan, maandishi ya ujumbe wa Mkurugenzi wa Hawza nchini Iram, Ayatullah A'rafi, kwenye hafla ya ufunguzi wa ofisi ya Shirika la Habari la Hawza katika Mkoa wa Golestan, ambayo yalisomwa na Hujjatul Islam wal Muslimin Rustami katika hafla hiyo iliyofanyika mjini Gorgan Iran, ni kama ifuatavyo:
Kwa Jina la Mwenyezi Mungu
Kwa kumshukuru na kumsifu Mwenyezi Mungu, na kwa kutuma salamu zisizo na kikomo kwa roho tukufu ya Rehema kwa walimwengu wote na Ahlu-Bayt wake watoharifu (as), pamoja na mashahidi wote wa Uislamu, hususan mashahidi wa Vita vya Tatu vya Kulazimishwa, akiwa mstari wao wa mbele Imam Shahidi, na kwa kumuombea afya njema na maisha marefu Kiongozi wa Umma, Ayatullah Sayyid Mujtaba Husseini Khamenei, na pia kwa kutoa heshima na taadhima kwa viongozi wote wakubwa na wahudhuriaji katika mkusanyiko huo wa kiroho na wa Hawza, pamoja na wananchi wote walioshiriki katika harakati hii kubwa ya ustaarabu.
Taasisi ya Hawza, ikiwa ni dhihirisho la madhehebu ya Ahlu-Bayt (as) na marejeo ya kielimu ya Mapinduzi ya Kiislamu, ni taasisi yenye mizizi ya kina miongoni mwa wananchi. Taasisi hii imejengwa juu ya misingi ya uhalisia, imani na urithi wa kale wa ustaarabu ambao katika historia yenye fahari ya Iran, umekuwa ukitoa bishara ya maisha, matumaini, ustawi, maendeleo na ukamilifu. Ni taasisi ambayo nguzo zake zote zimechanganyika na juhudi, uaminifu, hali ya kiroho na uelimishaji.
Wanazuoni na viongozi wakubwa wa dini, kama vinara wa harakati za mapambano, watetezi wa haki za wananchi na walinzi waaminifu wa mfumo wa Kiislamu, na zaidi ya yote walinzi wa mipaka ya fikra na utamaduni wa Sheria Tukufu, wamekuwa vielelezo vya kudumu vya maisha ya Kiislamu yaliyojaa imani, huku wakihimiza kudai haki sambamba na kuwajibika, kwa uadilifu na haki.
Kwa kuzingatia maelekezo ya Kiongozi Shahidi kuhusu kuifanya Hawza iwe taasisi iliyo mbele na bora, yenye ubunifu, inayokua, inayokwenda sambamba na wakati, inayojibu changamoto mpya, yenye maadili mema, yenye ari ya maendeleo na ya kijihadi, yenye utambulisho wa kimapinduzi, na pia yenye uwezo wa kubuni mifumo ya uendeshaji wa jamii, ni lazima pia Shirika la Habari la Hawza, kama dhihirisho la kimedia la Hawza na wanazuoni wake, kwa kufuata urithi huu mkubwa na wa thamani, liakisi maadili yote, huduma na mafanikio ya taasisi hii kubwa ya Hawza, na liwe jukwaa lililo wazi, lenye uwazi, linalotoa matumaini na lenye kuongoza washiriki wote wa sekta ya habari na uenezaji wa taarifa za kidini, pamoja na kuwa rejea ya kuaminika ya vyombo vya habari katika nyanja za utamaduni, imani na maadili katika dunia ya sasa.
Kuanzishwa kwa ofisi ya Shirika la Habari la Hawza, kwa juhudi za Kituo cha Vyombo vya Habari na Mtandao wa Hawza pamoja na uongozi wa Mkoa wa Golestan; mkoa ambao daima umekuwa miongoni mwa vinara wa mapambano dhidi ya ubeberu na ukoloni, na ardhi iliyopambwa kwa majina ya wanazuoni wakubwa wa dini, wafufuaji wa urithi mkubwa wa Ahlu-Bayt (as), mashahidi mashuhuri wa eneo hilo na watu maarufu wenye heshima kubwa, ni hatua inayostahili pongezi katika kuonesha taswira sahihi ya Hawza na wanazuoni, kuinua mjadala wa maadili na hali ya kiroho, pamoja na kuimarisha mahusiano kati ya Hawza na wananchi wa eneo hilo lenye historia ya fahari.
Inatarajiwa kwamba ofisi ya Shirika la Habari la Hawza ndani ya Golestan, kwa kutegemea uwezo mkubwa wa wanazuoni na wasomi, taasisi zote za Hawza, pamoja na kunufaika na uzoefu wa wake na waume wasomi, mbali na kuwasilisha kwa usahihi, uaminifu na busara huduma na mafanikio ya Hawza na taasisi zake katika mkoa huo, pia iwe chachu ya mabadiliko, ubunifu na maendeleo ya kielimu, na iwe kitovu cha wasomi na wataalamu wa fikra na utamaduni wa mkoa huo.
Kuimarisha Hawza katika mikoa ni miongoni mwa sera za msingi za uongozi wa Hawza, kupanua shughuli za Shirika la Habari la Hawza katika mikoa mbalimbali kunaweza kutoa mchango mkubwa katika kufanikisha lengo hili. Kwa msingi huo, tunaupokea kwa furaha kubwa ufunguzi wa ofisi ya Shirika la Habari la Hawza katika Mkoa wa Golestan, na tunawashukuru na kuwapongeza wapiganaji wote wa uwanja wa vyombo vya habari kwa juhudi zao.
Bila shaka, kuimarisha uwepo wa kielimu badala ya kujitosheleza na kuripoti matukio pekee, kuhifadhi historia simulizi ya mkoa, kuimarisha mawasiliano na taasisi za habari na vyombo vya habari, kuzipa umuhimu unaostahili taasisi zote za Hawza, kutoa uangalizi maalumu kwa Hawza ya wanawake na wanawake wasomi, kuwa na mtazamo wa kimataifa, na kuzalisha habari na bidhaa za kimedia kwa ubunifu, ni miongoni mwa vipaumbele muhimu ambavyo vinapaswa kupewa kipaumbele na Kituo cha Vyombo vya Habari na Mtandao pamoja na ofisi ya Shirika la Habari la Hawza katika mkoa.
Mwishoni, ninawashukuru kwa dhati na kuwathamini wanazuoni wote, wasomi, viongozi, wenye maoni na kalamu, pamoja na wapambanaji wote wa medani ya sanaa na vyombo vya habari, na wahudhuriaji wote waheshimiwa. Ninamuomba Mwenyezi Mungu awajaalie nyote mafanikio ya daima, na ninautakia Upande wa Haq pamoja na wapambanaji wote duniani nusura na ushindi.
Na mwisho wa dua yetu ni kwamba sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu wote.
Alireza A'rafi
Mkurugenzi wa Hawza nchini Iran.
Maoni yako